Monday, October 3, 2016

Taarifa kwa uma


NACTE

2ND OCTOBER 2016 22:35:00

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA AWAMU YA TATU, UHAMISHO NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA) KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Date Posted: 2nd October 2016 22:35:00 Posted By:NACTE

 

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

 (NACTE)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA AWAMU YA TATU, UHAMISHO NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA(CHETI) NA STASHAHADA(DIPLOMA) KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

 

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) na Umma kwa ujumla kuwa dirisha la maombi lilifungwa mnamo tarehe 15 Septemba 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa kozi hizo.

 

Uteuzi wa awamu ya tatu kwa waombaji wa Astashahada na Stashahada unatarajiwa kutangazwa mnamo tarehe 5 Oktoba 2016, hivyo basi waombaji wanaombwa kuwa na subira ili kutoa muda kwa Baraza kukamilisha taratibu za uteuzi huo.

 

Maombi mapya ya Udahili

Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) utafunguliwa tena tarehe 5 Oktoba 2016hadi tarehe 15 Oktoba 2016 ili kujaza nafasi za udahili zilizobaki wazi baada ya uchaguzi wa awamu ya pili. Hatua hii itawezesha kuruhusu machaguo mapya kwa wale ambao hawakuchaguliwa katika kozi walizoomba pamoja na kuruhusu waombaji wapya ambao kwa njia moja au nyingine hawakuweza kuomba hapo awali.

Maombi ya Uhamisho

Mwombaji aliyechaguliwa ataweza kuomba uhamisho kutoka chuo ama kozi moja kwenda nyingine kupitia kwenye ukurasa wake binafsi (profile) tu. Uhamisho huu utategemea nafasi zilizopoushindani naalama za chini za kujiunga na kozi (cut-off). Orodha ya Vyuo na Programu zenye nafasi zitatolewa hivi punde.

Hatua za kuomba uhamisho:

Ingia kwenye ukurasa wako binafsi (profile) kwa kutumia jina la mtumiaji (Username) na neno la siri (Password) ulivyopewa wakati wa usajili.

Bofya kitufye kilichoandikwa “Transfer Request/Kuomba uhamisho”, na punde ukurasa utafunguka

Utafunguka ukurasa unaokuonesha chuo na kozi uliyochaguliwa awali

Chagua kada unayohitaji kuhamia

Chagua chuo unachohitaji kuhamia

Chagua kozi unayohitaji kuhamia

Mfumo utatathmini kama una sifa za kujiunga na kozi uliyochagua. Iwapo una sifa za kujiunga na kozi hiyo mfumo utakuomba ulipie Sh. 30,000/- kama ada ya maombi ya uhamisho. Kiasi hiki hakitarudishwa (non-refundable)

Bofya kitufye kilichoandikwa “Confirm Transfer Request/Kamilisha maombi”.

Utapewa muhtasari wa maombi yako ya uhamisho pamoja na kutumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenye namba ya simu ya mkononi uliyoweka wakati wa usajili na barua pepe kukujulisha kwamba umekamilisha maombi.

Jinsi ya kulipia (Malipo yatafanywa kwa M- pesa tu)

Piga *150*00#

Chagua 4. LIPA kwa M-Pesa

Chagua 4. Weka namba ya kampuni

Tafadhali weka namba ya kampuni (No. 607070)

Weka namba ya kumbukumbu ya malipo (No. 1234)

Weka kiasi (e.g.30,000/=)

Weka namba ya siri

Bonyeza 1 kuthibitisha.

Angalizo (Disclaimer)

Kuhama chuo na kozi si lazima.

Uhamisho utafanyika kwa kozi zile tu zenye nafasi na kwa vyuo ambavyo bado havijafunguliwa na kuanza masomo.

Uhamisho ni kwa wale waombaji waliokwisha kuchaguliwa kupitia mfumo wa pamoja wa udahili tu.

Maombi ya uhamisho yanaweza kufanyika MARA MOJA na kwa kozi moja

Iwapo umefanikiwa kupata uhamisho, majibu yataonekana kwenye ukurasa wako binafsi (Profile). Majibu haya pia yatatumwa kwenye namba yako ya simu kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na kupitia barua pepe baada ya tarehe ya mwisho ya maombi (15 Oktoba 2016).

Uhamisho utategemea ufauluwa waombaji nanafasi zilizopo. Hii inamaanisha kwamba wenyeufaulu wa juu ndio wenye uwezo mkubwa wa kukubaliwa kuhama.

Maombi yatakayo tumwa kwa barua au barua pepe hayatoshughulikiwa.

Imetolewa na

Ofisi ya Katibu Mtendaji

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)

Tarehe: 02 Octoba, 2016

QUICK / RELATED LINKS

Central Admission SystemTanzania Commission for UniversitiesTanzania National WebsiteHigher Education Students Loans Board (HESLB)National Examination Council of Tanzania (NECTA)Tanzania Institute of Education (TIE)Commission for Science and TechnologyVocational Education Training Authority (VETA)International Association of Universities (IAU)Center for Higher Education Transformation (CHET)

Stay Connected

2kSHARES  1.5kTWEETS 620SHARES200FOLLOWERS

 

CONTACT NACTE

The Executive Secretary,The National Council For Technical Education:Plot No. 719/1/4,
Mikocheni Light Industrial Area,
P. O. Box 7109,
Dar-es-Salaam,
Tanzania.Tel: 255-22-2780077 / 255-22-2780079Fax: 255-22-2780060E-Mail: info@nacte.go.tzWebsite: www.nacte.go.tz

NACTE ZONES

LATEST UPDATES

 October 2nd 2016  NACTE

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA AWAMU YA TATU, UHAMISHO NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA) KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

 September 21st 2016  NACTE

PUBLIC NOTICE - ANNOUNCEMENT ON JOB VACANCY FOR THE POST OF EXECUTIVE SECRETARY OF THE COUNCIL

 September 14th 2016  NACTE

MATOKEO YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VYA UALIMU VYA SERIKALI KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

MORE UPDATES ...

NACTE TWEETER UPDATES

Tweets by @nacte

FOLLOW US ON FACEBOOK

HOME 

CONTACT GALLERY PUBLICATIONS

COPYRIGHT © 2007 - 2015 THE NATIONAL COUNCIL FOR TECHNICAL EDUCATION. ALL RIGHTS RESERVED
       WWW.stevedaboy.blogspot.com

No comments:

Post a Comment